Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 30:18 - Biblia Habari Njema

18 Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

18 Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Hata hivyo Mwenyezi Mungu anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonesha huruma. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Hata hivyo bwana anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa bwana ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

18 Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.

Tazama sura Nakili




Isaya 30:18
69 Marejeleo ya Msalaba  

Atakujibu vipi wakati wewe unasema kwamba humwoni na kwamba kesi yako iko mbele yake na wewe unamngojea!


msujudieni na kutetemeka; asije akakasirika, mkaangamia ghafla; kwani hasira yake huwaka haraka. Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!


Mtegemee Mwenyezi-Mungu! Uwe na moyo, usikate tamaa! Naam, mtegemee Mwenyezi-Mungu!


Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.


Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, heri mtu yule anayekutumainia wewe!


Ee mfalme mkuu, mpenda uadilifu! Umethibitisha haki katika Israeli; umeleta uadilifu na haki.


Kisha Mwenyezi-Mungu akapita mbele ya Mose akitangaza tena, “Mwenyezi-Mungu; mimi Mwenyezi-Mungu, ni Mungu mwenye huruma na neema; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhili na uaminifu.


Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu.


Maana, Mwenyezi-Mungu ameniambia hivi: “Toka makao yangu juu nitatazama yanayotukia, nimetulia kama joto katika mwanga wa jua, kama wingu la umande wakati wa mavuno.


Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa; na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.


Kiburi chote cha watu kitakomeshwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa. Na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.


Siku ile, watu wote watasema, “Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemngojea atuokoe. Huyu ndiye Mwenyezi-Mungu tuliyemtazamia. Njoni tufurahi na kushangilia kwa kuwa ametuokoa.”


Nitatumia haki kama kipimo changu, nitatumia uadilifu kupimia.” Mvua ya mawe itaufagilia mbali uongo mnaoutegemea, na mafuriko yataharibu kinga yenu.


Ee Mwenyezi-Mungu, utuonee huruma, kwako tumeliweka tumaini letu. Uwe kinga yetu kila siku, wokovu wetu wakati wa taabu.


Mwenyezi-Mungu ametukuka, yeye anaishi juu mbinguni. Ameujaza Siyoni haki na uadilifu.


Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.


Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza, nimekaa kimya na kujizuia; lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua, anayetweta pamoja na kuhema.


“Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu, nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui. Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga, na mahali pa kuparuza patakuwa laini. Huo ndio mpango wangu wa kufanya, nami nitautekeleza.


“Kwa heshima ya jina langu, ninaiahirisha hasira yangu; kwa ajili ya heshima yangu, ninaizuia nisije nikakuangamiza.


Lakini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atatukuzwa. Yeye huonesha ukuu wake kwa matendo yake ya haki, kwa kuwahukumu watu wake.


Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mawazo yangu si kama mawazo yenu, wala njia zangu si kama njia zenu.


Maana sitaendelea kuwalaumu wala kuwakasirikia daima. La sivyo hao niliowaumba watadhoofika mbele yangu, nami ndiye niliyewapa pumzi yangu ya uhai.


“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyanganyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.


Tangu kale hakuna aliyepata kuona wala kusikia kwa masikio yake; hakuna aliyepata kumwona Mungu aliye kama wewe atendaye mambo kwa ajili ya wale wanaomtegemea!


Nitamngojea Mwenyezi-Mungu ambaye amejificha mbali na wazawa wa Yakobo; nitamtumainia.


“Abarikiwe mtu anayemtegemea Mwenyezi-Mungu, mtu ambaye Mwenyezi-Mungu ndiye tegemeo lake.


Baada ya siku kumi, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia.


Heri yao watakaostahimili mpaka siku zile 1,335 zitakapotimia.


Lakini nitawahurumia watu wa Yuda na kuwaokoa. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, nitawaokoa, lakini si kwa nguvu za kijeshi, au pinde, au panga, au farasi au wapandafarasi.”


Kwa hiyo, nitamshawishi, nitampeleka jangwani na kusema naye kwa upole.


Nitarudi mahali pangu na kujitenga nao mpaka wakiri kosa lao na kunirudia. Taabu zao zitawafundisha wanitafute, wakisema:


Mmemchosha Mwenyezi-Mungu kwa maneno yenu matupu. Hata hivyo, mnasema, “Tumemchoshaje?” Mmemchosha mnaposema, “Mwenyezi-Mungu huwaona kuwa wema watu wanaotenda maovu; tena anawapenda.” Au mnapouliza, “Yuko wapi yule Mungu mwenye haki?”


Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.


Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.


Huyu ndiye yule aliyekwezwa na Mungu mpaka upande wake wa kulia, akawa kiongozi na Mwokozi, ili awawezeshe watu wa Israeli watubu, wapate kusamehewa dhambi zao.


Sheria ilitokea, ikasababisha kuongezeka kwa uhalifu; lakini pale dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi.


Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu. Alitaka kuonesha ghadhabu yake na kujulisha uwezo wake. Basi, alikuwa na saburi sana, akiwavumilia wale ambao walikuwa lengo la ghadhabu yake, ambao walistahili kuangamizwa.


Basi, tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu ambayo ametujalia katika Mwanae mpenzi!


aliyotukirimia bila kipimo! Kwa hekima na ujuzi wake wote


“Mwenyezi-Mungu ni Mwamba wa usalama; kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni za haki. Yeye ni Mungu mwaminifu asiye na kosa, yeye hufanya mambo ya uadilifu na ya haki.


Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.


Mnapaswa kuuona uvumilivu wa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni mpate kuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzi alivyowaandikia akitumia hekima aliyopewa na Mungu.


Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu.


Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo