Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 50:4 - Biblia Habari Njema

4 Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

4 Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Bwana Mungu Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa, ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka. Huniamsha asubuhi kwa asubuhi, huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa, ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka. Huniamsha asubuhi kwa asubuhi, huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

4 Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza.

Tazama sura Nakili




Isaya 50:4
31 Marejeleo ya Msalaba  

Maneno yako yamewainua waliokufa moyo, umewaimarisha waliokosa nguvu.


Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako.


Asubuhi unioneshe fadhili zako, maana nimekuwekea tumaini langu. Unifundishe mwenendo wa kufuata, maana nakuelekezea ombi la moyo wangu.


Ndipo niliposema: “Niko tayari; ninayotakiwa kufanya yameandikwa katika kitabu cha sheria;


Wewe u mzuri kuliko wanadamu wote, maneno yako ni fadhili tupu. Kwa hiyo Mungu amekubariki milele.


Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu, asubuhi nakutolea tambiko yangu, kisha nangojea unijibu.


Lakini mimi nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu; kila asubuhi nakuletea ombi langu.


Wasiwasi moyoni humkosesha mtu raha, lakini neno jema humchangamsha.


Kutoa jibu sahihi hufurahisha; neno lifaalo kwa wakati wake ni jema mno!


Neno lisemwalo wakati unaofaa, ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha.


Kila litakapopitia kwenu litawakumba; nalo litapita kila asubuhi, mchana na usiku. Kusikia ujumbe huu tu kutakuwa kitisho.


Wao wananidhihaki na kuuliza: “Huyu nabii ataka kumfundisha nani? Je, anadhani atatueleza sisi ujumbe wake? Je, sisi ni watoto wachanga walioachishwa kunyonya juzijuzi?


Hapo vipofu wataona tena, na viziwi watasikia tena.


Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu.


Nani kati yenu amchaye Mwenyezi-Mungu? Nani anayetii maneno ya mtumishi wake? Kama yupo atembeaye gizani bila taa, amtumainie Mwenyezi-Mungu, na kumtegemea Mungu wake.


“Watu wako watafunzwa nami Mwenyezi-Mungu, wanao watapata ustawi mwingi.


Nitalihifadhi agizo hilo na kulifunga fundisho hilo miongoni mwa wafuasi wangu.


Kisha Mwenyezi-Mungu akaunyosha mkono wake, akagusa kinywa changu, akaniambia, “Tazama nimeyatia maneno yangu kinywani mwako.


Waliochoka nitawachangamsha, na walegevu nitawapa nguvu.


“Kila siku asubuhi mtamtolea Mwenyezi-Mungu mwanakondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, ambaye atateketezwa mzima.


Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.


akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi lao hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?


Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.


kwa sababu mimi mwenyewe nitawapeni ufasaha wa maneno na hekima, hata maadui zenu hawataweza kustahimili wala kupinga.


Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”


Walinzi wakawajibu, “Hakuna mtu aliyepata kamwe kusema kama asemavyo mtu huyu!”


Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Wamesema ukweli.


Nitawateulia miongoni mwa ndugu zao wenyewe nabii kama wewe; nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo