Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yoshua 21:8 - Swahili Revised Union Version

Kisha wana wa Israeli waliwapa Walawi kwa kura miji hiyo pamoja na mbuga zake za malisho, kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Waisraeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na vijiji vya malisho yao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Waisraeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na vijiji vya malisho yao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Waisraeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na vijiji vya malisho yao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii na maeneo ya malisho ya kila mji, kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru kupitia kwa Musa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vile bwana alivyokuwa ameamuru kupitia kwa Musa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha wana wa Israeli waliwapa Walawi kwa kura miji hiyo pamoja na mbuga zake za malisho, kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yoshua 21:8
11 Marejeleo ya Msalaba  

Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri.


Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.


Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.


Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.


hao wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakamwendea Musa na Eleazari kuhani, na wakuu wa mkutano, wakanena nao, wakisema,


Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama makabila ya baba zenu yalivyo.


Hiyo miji watakuwa nayo ili wakae humo, na malisho watakuwa nayo kwa wanyama wao wa mifugo, na kwa mali zao, na kwa wanyama wao wote.


Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele ya BWANA, Mungu wetu.


Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na mbuga zake za malisho, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya BWANA.


Na wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao walipata miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi, na katika kabila la Zabuloni.


Kisha wakawapa katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, miji hii iliyotajwa hapa kwa majina;