Baba zetu katika Misri Hawakuzingatia matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, Bahari ya Shamu.
Yohana 10:6 - Swahili Revised Union Version Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa mambo hayo aliyowaambia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia. Neno: Bibilia Takatifu Isa alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia. Neno: Maandiko Matakatifu Isa alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia. BIBLIA KISWAHILI Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa mambo hayo aliyowaambia. |
Baba zetu katika Misri Hawakuzingatia matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, Bahari ya Shamu.
Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.
Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.
wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.
Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa inakuja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.
Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia?
Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.
Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.