Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka;
Mwanzo 1:6 - Swahili Revised Union Version Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” Biblia Habari Njema - BHND Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” Neno: Bibilia Takatifu Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji, igawe maji na maji.” Neno: Maandiko Matakatifu Mwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” BIBLIA KISWAHILI Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. |
Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka;
Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
Mawingu yakiwa yamejaa mvua, Yataimimina juu ya nchi; Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.
Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;