Methali 8:14 - Swahili Revised Union Version Ushauri ni wangu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nina uwezo wa kushauri na nina hekima. Ninao ujuzi na nina nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Nina uwezo wa kushauri na nina hekima. Ninao ujuzi na nina nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nina uwezo wa kushauri na nina hekima. Ninao ujuzi na nina nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu. BIBLIA KISWAHILI Ushauri ni wangu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. |
Hayo nayo yatoka kwa BWANA wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.
Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonesha njia ya fahamu?
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wagiriki, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;