Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
Methali 30:8 - Swahili Revised Union Version Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniondolee uongo na udanganyifu; usinipe umaskini wala utajiri; unipatie chakula ninachohitaji, Biblia Habari Njema - BHND Uniondolee uongo na udanganyifu; usinipe umaskini wala utajiri; unipatie chakula ninachohitaji, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniondolee uongo na udanganyifu; usinipe umaskini wala utajiri; unipatie chakula ninachohitaji, Neno: Bibilia Takatifu Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. Neno: Maandiko Matakatifu Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. BIBLIA KISWAHILI Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. |
Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme, siku kwa siku sehemu, siku zote za maisha yake.
Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao BWANA amewapa ninyi, mle.
Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.
Angalieni, kwa kuwa BWANA amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba.
Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arubaini, hata walipofikia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikia mipakani mwa nchi ya Kanaani.
Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
Hakuna anayeshitaki kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
Ndipo Sedekia mfalme akatoa amri, wakamtia Yeremia katika ukumbi wa walinzi; wakampa kila siku mkate mmoja uliotoka katika njia ya waokaji, hata mkate wote wa mji ulipokwisha. Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.
Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme wa Babeli; kila siku alipewa posho hata siku ya kufa kwake, siku zote za maisha yake.
wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; tunawahubiria Habari Njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;