Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 59:4 - Swahili Revised Union Version

4 Hakuna anayeshitaki kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Hakuna atoaye madai yake kwa haki, wala anayeshtaki kwa uaminifu. Mnategemea hoja batili; mnasema uongo. Mnatunga hila na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Hakuna atoaye madai yake kwa haki, wala anayeshtaki kwa uaminifu. Mnategemea hoja batili; mnasema uongo. Mnatunga hila na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Hakuna atoaye madai yake kwa haki, wala anayeshtaki kwa uaminifu. Mnategemea hoja batili; mnasema uongo. Mnatunga hila na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki; hakuna hata mmoja anayetetea kwa haki. Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo, huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki; hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki. Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo, huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Hakuna anayedai kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:4
36 Marejeleo ya Msalaba  

Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake.


Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Na mioyo yao hutunga udanganyifu.


BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi;


Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.


Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani.


Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoichimba!


Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.


Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao sheria za kudhulumu;


Tumekuwa na mimba, tumekuwa na uchungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.


Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;


Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali;


Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo;


Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA;


Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe.


Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?


Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.


Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari!


Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.


Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki.


Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.


Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona uovu.


Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu.


Mzee mwenye kuheshimiwa ndiye kichwa, na nabii afundishaye uongo ndiye mkia.


Maana, kwa kuwa umeyatumainia matendo yako, na hazina zako, wewe nawe utatwaliwa; na Kemoshi atatoka aende katika uhamisho, makuhani wake na wakuu wake pamoja.


Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.


Msitumainie maneno ya uongo, mkisema, Hekalu la BWANA, Hekalu la BWANA, Hekalu la BWANA ndiyo haya.


Angalieni, mnatumainia maneno ya uongo, yasiyoweza kufaidi.


Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.


Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.


Wayahudi nao wakamshitaki, wakisema ya kuwa ndivyo yalivyo.


Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo