Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.
Methali 3:7 - Swahili Revised Union Version Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu. Biblia Habari Njema - BHND Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu. Neno: Bibilia Takatifu Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Mwenyezi Mungu ukajiepushe na uovu. Neno: Maandiko Matakatifu Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche bwana ukajiepushe na uovu. BIBLIA KISWAHILI Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. |
Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.
Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.
Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.
Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.
Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.