Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 3:7 - Swahili Revised Union Version

7 Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Mwenyezi Mungu ukajiepushe na uovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche bwana ukajiepushe na uovu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.

Tazama sura Nakili




Methali 3:7
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.


Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.


Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.


Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.


Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.


Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.


Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.


Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.


Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.


Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.


Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.


Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.


Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.


Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.


Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.


Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!


Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.


Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo