Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 12:20 - Swahili Revised Union Version

20 Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Kisha, Daudi aliinuka kutoka sakafuni, akaoga, akajipaka mafuta na kubadilisha mavazi yake. Halafu akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuabudu. Kisha akarudi nyumbani na alipotaka chakula, akapewa, naye akala.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Kisha, Daudi aliinuka kutoka sakafuni, akaoga, akajipaka mafuta na kubadilisha mavazi yake. Halafu akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuabudu. Kisha akarudi nyumbani na alipotaka chakula, akapewa, naye akala.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Kisha, Daudi aliinuka kutoka sakafuni, akaoga, akajipaka mafuta na kubadilisha mavazi yake. Halafu akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuabudu. Kisha akarudi nyumbani na alipotaka chakula, akapewa, naye akala.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Basi Daudi akainuka kutoka pale sakafuni. Baada ya kuoga, akajipaka mafuta na kubadilisha nguo zake kisha akaenda ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, akaabudu. Baada ya hapo akaenda nyumbani mwake, akaomba wamwandalie chakula, naye akala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Basi Daudi akainuka kutoka pale sakafuni. Baada ya kuoga, akajipaka mafuta na kubadilisha nguo zake kisha akaenda ndani ya nyumba ya bwana, akaabudu. Baada ya hapo akaenda nyumbani kwake kwa kutaka kwake, wakamwandalia chakula, naye akala.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 12:20
20 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini alipoona ya kuwa watumishi wake wananong'onezana, Daudi alitambua ya kuwa mtoto amekufa; basi Daudi akawauliza watumishi wake, Je! Mtoto amekufa? Nao wakasema, Amekufa.


Watumishi wake wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto, alipokuwa hai; lakini mtoto alipokuwa amekufa, uliinuka ukala chakula.


Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unaomboleza, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki;


Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.


Wakaliingiza sanduku la BWANA, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.


Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele za BWANA, akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?


Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;


Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.


Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.


BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.


Nimenyamaza, sifumbui kinywa changu, Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.


Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.


Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.


Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose manukato.


Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;


Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.


Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; lakini usijioneshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa.


Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA.


Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo