Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Methali 28:18 - Swahili Revised Union Version Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aishiye kwa unyofu atasalimishwa, lakini mdanganyifu ataanguka kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Aishiye kwa unyofu atasalimishwa, lakini mdanganyifu ataanguka kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aishiye kwa unyofu atasalimishwa, lakini mdanganyifu ataanguka kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula. BIBLIA KISWAHILI Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara. |
Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.
Malaika wa BWANA akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,
Malaika wa BWANA akamwambia Balaamu Nenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki.
Lakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nilimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Lakini usipokesha, nitakuja kama mwizi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.