Methali 27:20 - Swahili Revised Union Version Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuzimu na Uharibifu kamwe havishibi, kadhalika na macho ya watu hayashibi. Biblia Habari Njema - BHND Kuzimu na Uharibifu kamwe havishibi, kadhalika na macho ya watu hayashibi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuzimu na Uharibifu kamwe havishibi, kadhalika na macho ya watu hayashibi. Neno: Bibilia Takatifu Kuzimu na Uharibifu havishibi, wala macho ya mwanadamu hayashibi. Neno: Maandiko Matakatifu Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. BIBLIA KISWAHILI Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. |
Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.
Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.
Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu.
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.