Methali 23:4 - Swahili Revised Union Version Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa unayo hekima ya kutosha, usijitaabishe kutafuta utajiri. Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa unayo hekima ya kutosha, usijitaabishe kutafuta utajiri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa unayo hekima ya kutosha, usijitaabishe kutafuta utajiri. Neno: Bibilia Takatifu Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonesha kujizuia. Neno: Maandiko Matakatifu Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonyesha kujizuia. BIBLIA KISWAHILI Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe. |
Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Kuna balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima;
Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
Nena, BWANA asema hivi, Mizoga ya watu itaanguka kama samadi juu ya mashamba, Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye, wala hapana mtu atakayeikusanya.
na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.