Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mhubiri 5:13 - Swahili Revised Union Version

13 Kuna balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Tena, nimeona jambo moja ovu sana duniani: Mtu alijirundikia mali ikawa hatari kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Tena, nimeona jambo moja ovu sana duniani: Mtu alijirundikia mali ikawa hatari kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Tena, nimeona jambo moja ovu sana duniani: mtu alijirundikia mali ikawa hatari kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Nimeshaona uovu mzito chini ya jua: Utajiri uliolimbikizwa na kuleta madhara kwa mwenye mali;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Nimeshaona uovu mzito chini ya jua: Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima na kuleta madhara kwa mwenye mali,

Tazama sura Nakili




Mhubiri 5:13
29 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akarudisha mali zote, akamrudisha Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.


Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.


Lakini mkewe Lutu, akiwa nyuma ya mumewe, aliangalia nyuma akawa nguzo ya chumvi.


Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataokoa chochote kutoka hicho alichokifurahia.


Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.


Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.


Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti.


Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.


Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Ladumu tangu kizazi hata kizazi?


Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.


na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake.


Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.


Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojitengenezea ili kuziabudu, kwa fuko na popo;


Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.


Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.


Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo