Methali 22:5 - Swahili Revised Union Version Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njia ya waovu imejaa miiba na mitego; anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa. Biblia Habari Njema - BHND Njia ya waovu imejaa miiba na mitego; anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njia ya waovu imejaa miiba na mitego; anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa. Neno: Bibilia Takatifu Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego, bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo. Neno: Maandiko Matakatifu Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego, bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo. BIBLIA KISWAHILI Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo. |
Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.
Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.
Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.
Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi.
Tunajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.