Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Methali 21:16 - Swahili Revised Union Version Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu. Biblia Habari Njema - BHND Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu. Neno: Bibilia Takatifu Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa. BIBLIA KISWAHILI Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa. |
Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.
Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.
na hao waliorudi nyuma, na kuacha kumfuata BWANA; na hao wasiomtafuta BWANA, wala kumwulizia.
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;