Methali 18:7 - Swahili Revised Union Version Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kinywa cha mpumbavu humwangamiza mwenyewe; mdomo wake ni mtego wa kumnasa yeye mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Kinywa cha mpumbavu humwangamiza mwenyewe; mdomo wake ni mtego wa kumnasa yeye mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kinywa cha mpumbavu humwangamiza mwenyewe; mdomo wake ni mtego wa kumnasa yeye mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake. BIBLIA KISWAHILI Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake. |
Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa; Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu. Wote wawaonao watatikisa kichwa.
Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.
Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.