Methali 15:24 - Swahili Revised Union Version Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njia ya mwenye hekima huelekea juu kwenye uhai, ili aepe kuingia chini kuzimu. Biblia Habari Njema - BHND Njia ya mwenye hekima huelekea juu kwenye uhai, ili aepe kuingia chini kuzimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njia ya mwenye hekima huelekea juu kwenye uhai, ili aepe kuingia chini kuzimu. Neno: Bibilia Takatifu Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima kumwepusha asiende chini kaburini. Neno: Maandiko Matakatifu Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima kumwepusha asiende chini kaburini. BIBLIA KISWAHILI Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini. |
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
Nawe waambie watu hawa, BWANA asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;