Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 4:18 - Swahili Revised Union Version

18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri, ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri, ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri, ambayo hung'aa zaidi na zaidi hata mchana kamili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hung’aa zaidi na zaidi hadi mchana mkamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hung’aa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.

Tazama sura Nakili




Methali 4:18
25 Marejeleo ya Msalaba  

Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu. Likichipuza mimea ardhini, Kwa mwangaza baada ya mvua;


Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Giza lake litakuwa kama alfajiri.


Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.


Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.


Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.


Nuru humwangazia mwenye haki, Na furaha ni kwa wanyofu wa moyo.


Nuru ya mwenye haki yang'aa sana; Bali taa ya mtu mbaya itazimika.


Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.


Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki.


Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema.


Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.


Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.


Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.


Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji ukiwa juu ya mlima hauwezi kusitirika.


Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.


Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.


mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,


Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.


Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.


Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.


Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arubaini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo