Methali 14:23 - Swahili Revised Union Version Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini. Biblia Habari Njema - BHND Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini. Neno: Bibilia Takatifu Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. Neno: Maandiko Matakatifu Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. BIBLIA KISWAHILI Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. |
Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.