Methali 13:23 - Swahili Revised Union Version Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shamba la maskini hutoa mazao mengi, lakini bila haki hunyakuliwa. Biblia Habari Njema - BHND Shamba la maskini hutoa mazao mengi, lakini bila haki hunyakuliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shamba la maskini hutoa mazao mengi, lakini bila haki hunyakuliwa. Neno: Bibilia Takatifu Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi, bali dhuluma hukifutilia mbali. Neno: Maandiko Matakatifu Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi, bali dhuluma hukifutilia mbali. BIBLIA KISWAHILI Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma. |
Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba.
wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo yake humo bondeni;