Methali 13:16 - Swahili Revised Union Version Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili, lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili, lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili, lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake. Neno: Bibilia Takatifu Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa, bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa, bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake. BIBLIA KISWAHILI Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. |
Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.
Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.
Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Maana utii wenu umewafikia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wasio na hatia katika mambo mabaya.
Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu muwe watu wazima.
Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.
Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.