Methali 12:3 - Swahili Revised Union Version Mtu hatathibitika kwa njia ya uovu; Shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu hawi imara kwa kutenda maovu, lakini hakuna kiwezacho kumngoa mtu mwadilifu. Biblia Habari Njema - BHND Mtu hawi imara kwa kutenda maovu, lakini hakuna kiwezacho kumngoa mtu mwadilifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu hawi imara kwa kutenda maovu, lakini hakuna kiwezacho kumng'oa mtu mwadilifu. Neno: Bibilia Takatifu Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa. BIBLIA KISWAHILI Mtu hatathibitika kwa njia ya uovu; Shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe. |
Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuponyoka katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.