Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Methali 12:12 - Swahili Revised Union Version Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waovu hutamani faida isiyo halali, lakini mtu mwadilifu husimama imara. Biblia Habari Njema - BHND Waovu hutamani faida isiyo halali, lakini mtu mwadilifu husimama imara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waovu hutamani faida isiyo halali, lakini mtu mwadilifu husimama imara. Neno: Bibilia Takatifu Waovu hutamani mateka ya wapotovu, bali shina la mwenye haki hustawi. Neno: Maandiko Matakatifu Waovu hutamani mateka ya watu wabaya, bali shina la mwenye haki hustawi. BIBLIA KISWAHILI Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda. |
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.
Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
Na mabaki yaliyookoka, yaliyobakia ya nyumba ya Yuda, yatatia mizizi chini, na kuzaa matunda juu.
Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.