Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Methali 11:7 - Swahili Revised Union Version Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake linapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka; tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu. Biblia Habari Njema - BHND Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka; tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka; tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu. Neno: Bibilia Takatifu Matumaini yaliyo katika wanadamu hufa pamoja nao; ahadi zote za uwezo wao hubatilika. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu. BIBLIA KISWAHILI Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake linapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. |
Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha.