BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
Methali 11:4 - Swahili Revised Union Version Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo. Biblia Habari Njema - BHND Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo. Neno: Bibilia Takatifu Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. Neno: Maandiko Matakatifu Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. BIBLIA KISWAHILI Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. |
BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.
Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya BWANA; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.