Methali 10:8 - Swahili Revised Union Version Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye hekima moyoni hutii amri, lakini mpumbavu aropokaye ataangamia. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye hekima moyoni hutii amri, lakini mpumbavu aropokaye ataangamia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye hekima moyoni hutii amri, lakini mpumbavu aropokaye ataangamia. Neno: Bibilia Takatifu Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. BIBLIA KISWAHILI Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka. |
mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.
Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.