Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Methali 10:28 - Swahili Revised Union Version Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali matarajio yao wasio haki yatapotea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha, lakini tazamio la mwovu huishia patupu. Biblia Habari Njema - BHND Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha, lakini tazamio la mwovu huishia patupu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha, lakini tazamio la mwovu huishia patupu. Neno: Bibilia Takatifu Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu. Neno: Maandiko Matakatifu Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu. BIBLIA KISWAHILI Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali matarajio yao wasio haki yatapotea. |
Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mwimbieni wimbo yeye apitaye katika mawingu, Jina lake ni YAHU; Shangilieni mbele zake.
Haja ya mwenye haki ni kupata mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu huishia katika ghadhabu.
Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,