Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
Mathayo 7:28 - Swahili Revised Union Version Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake. Biblia Habari Njema - BHND Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake. Neno: Bibilia Takatifu Isa alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, Neno: Maandiko Matakatifu Isa alipomaliza kusema maneno haya, makutano ya watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, BIBLIA KISWAHILI Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; |
Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.
Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika katika eneo la Yudea, ng'ambo ya Yordani.
mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi.
Wakuu wa makuhani na waandishi wakapata habari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza; maana walimwogopa, kwa sababu mkutano wote walishangazwa na mafundisho yake.
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?