Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,
Mathayo 4:12 - Swahili Revised Union Version Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya. Neno: Bibilia Takatifu Isa aliposikia kwamba Yahya alikuwa amefungwa gerezani, alirudi Galilaya. Neno: Maandiko Matakatifu Isa aliposikia kwamba Yahya alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. BIBLIA KISWAHILI Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; |
Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,
Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye.
Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu,
Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo, ndugu yake, kwa kuwa amemwoa;
Nao walisisitiza sana, wakisema, Huwataharakisha watu, akifundisha katika Yudea yote, tokea Galilaya mpaka huku.
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaendea Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Kesho yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.
Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.