Maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi, katika nchi ya Benyamini;
Mathayo 16:14 - Swahili Revised Union Version Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane Mbatizaji, wengine Elia, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.” Biblia Habari Njema - BHND Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane Mbatizaji, wengine Elia, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane Mbatizaji, wengine Elia, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.” Neno: Bibilia Takatifu Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yahya; wengine husema ni Ilya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmoja wa manabii.” Neno: Maandiko Matakatifu Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yahya; wengine husema ni Ilya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.” BIBLIA KISWAHILI Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. |
Maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi, katika nchi ya Benyamini;
Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika.
Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake.
Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama mmoja wa manabii.
na wengine ya kwamba Eliya ametokea, na wengine ya kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.
Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje kuhusu habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.