Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yohana 1:21 - Swahili Revised Union Version

21 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Hapo wakamwuliza, “Basi, wewe ni nani? Je, wewe ni Elia?” Yohane akajibu, “La, mimi siye.” Wakamwuliza, “Je, wewe ni yule nabii?” Yohane akawajibu, “La!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Hapo wakamwuliza, “Basi, wewe ni nani? Je, wewe ni Elia?” Yohane akajibu, “La, mimi siye.” Wakamwuliza, “Je, wewe ni yule nabii?” Yohane akawajibu, “La!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Hapo wakamwuliza, “Basi, wewe ni nani? Je, wewe ni Elia?” Yohane akajibu, “La, mimi siye.” Wakamwuliza, “Je, wewe ni yule nabii?” Yohane akawajibu, “La!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Wakamuuliza, “Wewe ni nani, basi? Je, wewe ni Ilya?” Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Je, wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Ilya?” Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Je, wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Wakamwuliza, Ni nani basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:21
12 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika.


Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.


Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.


Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.


Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotayarishwa.


Basi wakamwambia, U nani? Na tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wanenaje juu yako mwenyewe?


Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?


Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.


Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo