Basi, viongozi wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale tisa wakae mijini.
Isaya 48:2 - Swahili Revised Union Version Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; BWANA wa majeshi ni jina lake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyinyi mnaona fahari kujiita watu wa mji mtakatifu, na kujidai kumtegemea Mungu wa Israeli, ambaye jina lake ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Biblia Habari Njema - BHND Nyinyi mnaona fahari kujiita watu wa mji mtakatifu, na kujidai kumtegemea Mungu wa Israeli, ambaye jina lake ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyinyi mnaona fahari kujiita watu wa mji mtakatifu, na kujidai kumtegemea Mungu wa Israeli, ambaye jina lake ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Neno: Bibilia Takatifu ninyi mnaojiita raia wa mji mtakatifu, na kumtegemea Mungu wa Israeli, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake: Neno: Maandiko Matakatifu ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu, na kumtegemea Mungu wa Israeli, bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: BIBLIA KISWAHILI Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; BWANA wa majeshi ni jina lake. |
Basi, viongozi wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale tisa wakae mijini.
Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
Tena itakuwa katika siku hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, bali watamtegemea BWANA, Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli.
Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.
Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
Tafadhali utuulizie habari kwa BWANA; kwa maana Nebukadneza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda BWANA atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, na kumfanya aende zake akatuache.
Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema BWANA, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo!
Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kumaliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia mhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.
nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Na behewa lililo nje ya hekalu uliache nje wala usilipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
Ndipo Mika akasema, Sasa ninajua ya kwamba BWANA atanitendea mema, kwa kuwa nina Mlawi kama kuhani wangu.