Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 47:4 - Swahili Revised Union Version

4 Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Mkombozi wetu: Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake; ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Mkombozi wetu: bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake; ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Isaya 47:4
12 Marejeleo ya Msalaba  

Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.


Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.


BWANA, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Kwa ajili yenu nimetuma ujumbe Babeli nami nitawashusha wote mfano wa wakimbizi, naam, Wakaldayo, katika merikebu zao walizozifurahia.


Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.


BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.


Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na watu wote watajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma.


Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.


Kwa maana BWANA amemweka huru Yakobo, amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye.


Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo