Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 10:16 - Swahili Revised Union Version

16 Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo, maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote, na Israeli ni taifa lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 10:16
28 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA ndiye aliye fungu langu, Ninaahidi kuyatii maneno yake.


Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa.


BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai.


Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.


Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.


Ulikumbuke kusanyiko lako, Ulilolinunua zamani. Ulilolikomboa liwe kabila la urithi wako, Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.


Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,


Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.


BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.


kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.


Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.


Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.


Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma.


Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.


Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.


Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.


BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;


wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;


BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi,


Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.


Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.


Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.


BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.


Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.


Na BWANA atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena.


Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo