Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 3:11 - Swahili Revised Union Version

11 Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea Mwenyezi Mungu na kusema, “Je, Mwenyezi Mungu si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea bwana na kusema, “Je, bwana si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.

Tazama sura Nakili




Mika 3:11
39 Marejeleo ya Msalaba  

Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu.


Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wezi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawafikii.


Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; BWANA wa majeshi ni jina lake.


wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake!


Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.


Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wowote.


Na makuhani, na manabii, na watu wote, wakamsikia Yeremia, hapo aliposema maneno haya katika nyumba ya BWANA.


Wamemkataa BWANA, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa;


Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.


Msitumainie maneno ya uongo, mkisema, Hekalu la BWANA, Hekalu la BWANA, Hekalu la BWANA ndiyo haya.


Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; maana kila mmoja wao, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa, ni mtamanifu; tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.


Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.


Wakuu wake kati yake wamekuwa kama mbwamwitu wakirarua mawindo; ili kumwaga damu, na kuharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.


Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?


Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu.


Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao.


Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo.


Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele.


BWANA asema hivi kuhusu manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.


Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.


Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.


Manabii wake ni watu hafifu, wadanganyifu; makuhani wake wamepatia unajisi patakatifu, wameifanyia sheria udhalimu.


Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.


Kwa sababu hiyo mimi nami nimewafanya ninyi kuwa kitu cha kudharauliwa, na unyonge, mbele ya watu wote, kama vile ninyi msivyozishika njia zangu, bali mmewapendelea watu katika sheria.


Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao.


Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.


wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.


asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi, wala asiwe mwenye kupenda fedha;


Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.


Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya malipo, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo