Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Amosi 8:4 - Swahili Revised Union Version Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikilizeni enyi mnaowakandamiza wanyonge na kuwaletea maangamizi fukara wa nchi. Biblia Habari Njema - BHND Sikilizeni enyi mnaowakandamiza wanyonge na kuwaletea maangamizi fukara wa nchi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikilizeni enyi mnaowakandamiza wanyonge na kuwaletea maangamizi fukara wa nchi. Neno: Bibilia Takatifu Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji, na kuwaonea maskini wa nchi, Neno: Maandiko Matakatifu Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji, na kuwaonea maskini wa nchi, BIBLIA KISWAHILI Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, |
Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.
Basi, lisikieni neno la BWANA, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.
Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; BWANA hakukutuma; lakini unawapa tumaini watu hawa kwa maneno ya uongo.
Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamuoni; mlio na masikio ila hamsikii.
Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.
Basi, kwa kuwa mnamkanyaga maskini, na kumtoza ngano; ninyi mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, lakini hamtakaa ndani yake; ninyi mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake.
Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Basi, sasa lisikie neno la BWANA; Wewe unasema, Usitabiri juu ya Israeli, wala usitoe neno lako juu ya nyumba ya Isaka;
Nao hutamani mashamba, na kuyanyakua; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.
Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani.
Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote;
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.