Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Nendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.
Yohana 2:5 - Swahili Revised Union Version Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.” Biblia Habari Njema - BHND Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.” Neno: Bibilia Takatifu Mama yake akawaambia wale watumishi, “Fanyeni lolote atakalowaambia.” Neno: Maandiko Matakatifu Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.” BIBLIA KISWAHILI Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni. |
Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Nendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.
Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nilitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao.
Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.
Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.