Yohana 2:2 - Swahili Revised Union Version Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Biblia Habari Njema - BHND naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Neno: Bibilia Takatifu Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. Neno: Maandiko Matakatifu Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. BIBLIA KISWAHILI Yesu naye alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. |
Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.
Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka katika nchi ya Yudea; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.
Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee chochote.
Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia?
Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.
Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Kumi na Wawili.
Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Yudea, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.
hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
Na wale wanafunzi, kila mtu kwa kadiri ya alivyofanikiwa, wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yudea.
Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yuko hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yuko huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu.
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.