Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;
Waebrania 12:6 - Swahili Revised Union Version Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humuonya Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Bwana humpa nidhamu kila anayempenda, humwadhibu kila anayekubali kuwa mwanawe.” Biblia Habari Njema - BHND Maana Bwana humpa nidhamu kila anayempenda, humwadhibu kila anayekubali kuwa mwanawe.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana Bwana humpa nidhamu kila anayempenda, humwadhibu kila anayekubali kuwa mwanawe.” Neno: Bibilia Takatifu kwa sababu Mwenyezi Mungu huwaadibisha wale anaowapenda, na humwadhibu kila mmoja anayemkubali kuwa mwana.” Neno: Maandiko Matakatifu kwa sababu Mwenyezi Mungu huwaadibisha wale awapendao, na humwadhibu kila mmoja anayemkubali kuwa mwana.” BIBLIA KISWAHILI Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. |
Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo BWANA, Mungu wako, akurudivyo.
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Angalieni, twawaita heri wao waliostahimili. Mmesikia habari za kustahimili kwake Ayubu, kuona mwisho Bwana aliyomtendea, jinsi Bwana alivyo mwingi wa rehema na mwenye huruma.