Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 5:4 - Swahili Revised Union Version Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka mia nane, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. BIBLIA KISWAHILI Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. |
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arubaini, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Adamu akaishi miaka mia moja na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia tano na tisini na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Wavulana wetu wakiwa ujanani wawe kama miche Iliyostawi kikamilifu. Binti zetu wawe kama nguzo za pembeni Zilizochongwa ili kupamba kasri.