Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Mwanzo 17:3 - Swahili Revised Union Version Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia, Biblia Habari Njema - BHND Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia, Neno: Bibilia Takatifu Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, Neno: Maandiko Matakatifu Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, BIBLIA KISWAHILI Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, |
Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka chini,
Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu.
Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akafunika uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Basi, nikaondoka, nikaenda bondeni, na tazama, utukufu wa BWANA ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Tena ikawa, walipokuwa wakiwaua, nami nikaachwa, nilianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
Lakini niliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi.
Nao wakaanguka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?
Akasema, La, lakini mimi ni kamanda wa jeshi la BWANA, nimekuja sasa. Yoshua akainama chini hadi nchi, akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
Kwa maana, ikawa, mara huo muali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa BWANA akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakaanguka kifudifudi.