Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 18:2 - Swahili Revised Union Version

2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka chini,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ibrahimu akainua macho, akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, akaharakisha kutoka ingilio la hema lake, akawalaki na kusujudu hadi chini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ibrahimu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka chini,

Tazama sura Nakili




Mwanzo 18:2
23 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia,


Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Abrahamu akaenda pamoja nao awasindikize.


Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Abrahamu alibaki amesimama mbele za BWANA.


akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.


Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.


Abrahamu akainama mbele ya watu wa nchi.


Abrahamu akaondoka, akainama mbele ya watu wa nchi, mbele ya hao wazawa wa Hethi.


Isaka akatoka ili kutafakari shambani wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.


Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.


Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.


Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka chini.


Wakasema, Mtumishi wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.


Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi.


Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudi


Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.


kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.


Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.


Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akainua macho yake na kuangalia juu, akaona ghafla mtu mmoja, mwanamume amesimama amemkabili naye alikuwa na upanga uliofutwa mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?


Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika;


Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume.


Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo