Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 18:1 - Swahili Revised Union Version

1 BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mwenyezi Mungu akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 18:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.


Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.


Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.


Mungu alipomaliza kusema naye, akaondoka kwa Abrahamu.


Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Abrahamu alibaki amesimama mbele za BWANA.


Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.


BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.


Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.


Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,


Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe.


Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.


Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani,


Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.


Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.


Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akainua macho yake na kuangalia juu, akaona ghafla mtu mmoja, mwanamume amesimama amemkabili naye alikuwa na upanga uliofutwa mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo