Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 14:5 - Swahili Revised Union Version

5 Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko la wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Hapo, Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya jumuiya yote ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Hapo, Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya jumuiya yote ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Hapo, Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya jumuiya yote ya Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko lote la Waisraeli waliokusanyika hapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko lote la Kiisraeli lililokusanyika hapo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko la wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Hesabu 14:5
18 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia,


Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu.


Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa BWANA amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusalemu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifudifudi, nao wamevaa nguo za magunia.


Tena ikawa, walipokuwa wakiwaua, nami nikaachwa, nilianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?


Lakini niliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi.


Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na yale mafuta juu ya madhabahu; watu wote walipouona huo moto wakapiga kelele wakainama kifudifudi.


Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;


Nao wakaanguka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?


Musa aliposikia maneno haya, akaanguka kifudifudi;


Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakaanguka kifudifudi.


Kisha BWANA akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung'uniko yao waliyoninung'unikia, ili wasife.


Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hadi mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea.


Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniondokee; lakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Akasema, La, lakini mimi ni kamanda wa jeshi la BWANA, nimekuja sasa. Yoshua akainama chini hadi nchi, akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?


BWANA akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?


ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao hutupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,


Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.


Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifudifudi mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo