Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mika 1:11 - Swahili Revised Union Version

Piteni; njia yenu, wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye aibu; Wakazi wa Saanani msitokeze nje; Beth-eseli unalia na ataondoa msaada wake kwenu;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nendeni enyi wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye haya. Wakazi wa Zaanani msitoke nje ya mji wenu. Watu wa Beth-ezeli wanalia; msaada wao kwenu umeondolewa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nendeni enyi wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye haya. Wakazi wa Zaanani msitoke nje ya mji wenu. Watu wa Beth-ezeli wanalia; msaada wao kwenu umeondolewa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nendeni enyi wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye haya. Wakazi wa Zaanani msitoke nje ya mji wenu. Watu wa Beth-ezeli wanalia; msaada wao kwenu umeondolewa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, ninyi mnaoishi Shafiri. Wale wanaoishi Saanani hawatatoka nje. Beth-Eseli iko katika maombolezo; kinga yake imeondolewa kwako.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, ninyi mkaao Shafiri. Wale waishio Saanani hawatatoka nje. Beth-Eseli iko katika maombolezo; kinga yake imeondolewa kwako.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Piteni; njia yenu, wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye aibu; Wakazi wa Saanani msijitokeze nje; Beth-eseli unalia na ataondoa msaada wake kwenu;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mika 1:11
12 Marejeleo ya Msalaba  

Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.


vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, bila viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.


Nawe ukisema moyoni mwako, Mbona mambo haya yamenipata mimi? Ni kwa sababu ya wingi wa uovu wako, marinda yako yamefunuliwa, na visigino vya miguu yako vimeumia.


Haya! Kimbieni! Jiokoeni nafsi zenu! Mkawe kama mtu aliye mkiwa.


Mpe Moabu mabawa, apate kuruka na kwenda zake; na miji yake itakuwa ukiwa, isiwe na mtu wa kukaa ndani yake.


basi, tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote.


nao watakutenda mambo kwa chuki, watakunyang'anya matunda yote ya kazi yako, watakuacha uchi, huna nguo na aibu ya mambo yako ya kikahaba itafunuliwa, uasherati wako na uzinzi wako.


Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi; Nitaomboleza kama mbweha, Na kulia kama mbuni.


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.


Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.


Senani, Hadasha, Migdal-gadi;