Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 48:9 - Swahili Revised Union Version

9 Mpe Moabu mabawa, apate kuruka na kwenda zake; na miji yake itakuwa ukiwa, isiwe na mtu wa kukaa ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mchimbieni Moabu kaburi, maana kuangamia kwake ni hakika; miji yake itakuwa tupu, bila mkazi hata mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mchimbieni Moabu kaburi, maana kuangamia kwake ni hakika; miji yake itakuwa tupu, bila mkazi hata mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mchimbieni Moabu kaburi, maana kuangamia kwake ni hakika; miji yake itakuwa tupu, bila mkazi hata mmoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, kwa kuwa ataangamizwa; miji yake itakuwa ukiwa, hakutakuwa na mtu atakayeishi ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, kwa kuwa ataangamizwa; miji yake itakuwa ukiwa, pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Mpe Moabu mabawa, apate kuruka na kwenda zake; na miji yake itakuwa ukiwa, isiwe na mtu wa kukaa ndani yake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 48:9
8 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu?


Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningeruka mbali na kustarehe.


Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.


Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.


Ee binti ukaaye katika Misri, Ujiweke tayari kwenda zako hali ya kufungwa; Kwa maana Nofu utakuwa ukiwa, Utateketezwa, usikaliwe na watu.


Enyi mkaao Moabu, ondokeni mijini, Nendeni mkakae majabalini; Mkawe kama njiwa atengenezaye kiota chake Kandoni mwa mdomo wa shimo.


Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.


Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo