Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 48:10 - Swahili Revised Union Version

10 Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Mwenyezi-Mungu kwa ulegevu; alaaniwe anayezuia upanga wake usimwage damu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Mwenyezi-Mungu kwa ulegevu; alaaniwe anayezuia upanga wake usimwage damu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Mwenyezi-Mungu kwa ulegevu; alaaniwe anayezuia upanga wake usimwage damu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Mwenyezi Mungu kwa ulegevu! Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya bwana kwa hila! Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!

Tazama sura Nakili




Yeremia 48:10
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa mfalme alipopita, alimwita mfalme; akasema, Mtumwa wako aliingia katikati ya pigano; na tazama, mtu mmoja akanigeukia akaniletea mtu, akaniambia, Umlinde mtu huyu; akipotea kwa njia yoyote, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, au utatoa talanta ya fedha.


Ikawa mtumishi wako alipokuwa akitenda haya na haya, yule akaenda zake. Mfalme wa Israeli akamwambia, Ndivyo itakavyokuwa hukumu yako; umejihukumu mwenyewe.


Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa sababu umemwachilia atoke mkononi mwako mtu niliyemweka ili aangamizwe kabisa, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, na watu wako mahali pa watu wake.


Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.


ukawaambie, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya,


Ee upanga wa BWANA, Siku ngapi zitapita kabla hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie.


Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo.


BWANA amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo.


Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.


lakini msikae ninyi; wafuatieni adui zenu, mwapige hao walio nyuma; msiwaache wakaingia ndani ya miji yao; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, amewatia mikononi mwenu.


Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.


Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.


Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo