Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 16:2 - Swahili Revised Union Version

2 Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao, ndivyo walivyo mabinti wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao, ndivyo walivyo mabinti wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao, ndivyo walivyo mabinti wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kiota, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Mto Arnoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kwenye kiota, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.

Tazama sura Nakili




Isaya 16:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Mesha, mfalme wa Moabu, alikuwa mfuga kondoo; naye alikuwa akimlipa mfalme wa Israeli wana-kondoo elfu mia moja na sufu ya kondoo dume elfu mia moja.


Kama shomoro katika kutangatanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpati mtu.


Kama ndege aendaye huku na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huku na huko mbali na mahali pake.


Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe.


Moabu ameaibishwa, kwa maana amevunjika; Ombolezeni na kulia; Tangazeni habari hii katika Arnoni, Ya kuwa Moabu ameharibika.


Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani.


Mpe Moabu mabawa, apate kuruka na kwenda zake; na miji yake itakuwa ukiwa, isiwe na mtu wa kukaa ndani yake.


Ole wako Moabu! Umeangamia, enyi watu wa Kemoshi; Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi, Na binti zake waende utumwani, Wamwendee Sihoni mfalme wa Waamori.


Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa na ngome ndefu ya kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea;


Na nchi hiyo tuliitwaa ikawa milki yetu, wakati huo; kutoka Aroeri iliyo kwenye bonde la Arnoni, na nusu ya nchi ya milima ya Gileadi, na miji iliyokuwamo, niliwapa Wareubeni na Wagadi;


Tukaitwaa na nchi wakati huo, katika mikono ya hao wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ng'ambo ya Yordani, kutoka bonde la Arnoni mpaka kilima cha Hermoni;


Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba;


Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo